Serikali
ya Tanzania imetoa uraia kwa wakimbizi 1,541 wa kisomali waliokuwa wanaishi
katika makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Watu
hao waliikimbia Somalia mwaka 1990 baada ya kuibuka kwa vita nchini mwao ambapo
3,000 kati ya waliokimbilia Tanzania walipokelewa na kuhifadhiwa katika kambi
ya Mkuyu iliyopo mkoani Tanga.
Watu
hao kwa kipindi chote hicho walikuwa wakipata msaada kutoka Shirika la
kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR).
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikwawe amesema wakimbizi hao ambao kwa
sasa ni raia wa Tanzania, walihamishwa na Serikali mwaka 2003 kutoka kambi ya
Mkuyu na kuja katika makazi ya Chogo ili wapatiwe mashamba kwa ajili ya
kujishughulisha na kilimo ili waweze kujitegemea.
Hata
hivyo, Waziri Chikawe amewataka wakimbizi 150 walioko katika makazi ya Chogo
ambao hawakuomba kuwa raia wa Tanzania kwa nia ya kurudi nchini kwao pale amani
itakapo patikana wanapaswa kuendelea kutii sheria za nchi zinazotawala hifadhi
ya ukimbizi nchini.
No comments:
Post a Comment