Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na
taasisi moja ya utafiti nchini Ufaransa yameonyesha kuwa Watunisia wengi
wanaunga mkono Uislamu kuwa na nafasi katika utungaji sheria za nchi yao.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, asilimia
51 ya wananchi wa Tunisia wanaitakidi kuwa Uislamu unapasa uwe moja ya vyanzo
vya utungaji sheria na uendeshaji serikali.
Asilimia 28 ya waliotoa maoni yao wamesema
wanahisi ni bora dini isiwe na nafasi katika suala la utungaji sheria.
Hii ni katika hali ambayo asilimia 16 ya raia
wa nchi hiyo wanataka Uislamu uwe ndio marejeo pekee ya utungaji sheria na
uendeshaji wa serikali hiyo.
Kuhusiana na aina ya utawala, uchunguzi huo wa
maoni aidha umeonyesha kuwa asilimia 52 ya raia wa Tunisia wanafadhilisha
serikali yenye mfumo wa kidemokrasia kuliko mifumo mingineyo, wakati asilimia
26 ya waliotoa maoni yao wanapendelea mifumo mingine ya utawala badala ya ule
wa kidemokrasia.
Kutokana na Watunisia wengi kutaka Uislamu uwe
moja ya vyanzo vya utungaji sheria na uendeshaji serikali, imedhihirika kuwa
wananchi hao wanaamini kwamba hakuna mgongano kati ya Uislamu na demokrasia na
bila uislamu demokrasia haiwezi kusimama.
No comments:
Post a Comment