G7 LAITISHIA RUSSIA KUIWEKEA VIKWAZO ZAIDI.
Kundi la
G7 la nchi zinazoongoza kwa viwanda duniani limetishia kuiwekea Russia vikwazo
zaidi kutokana na mgogoro wa Ukraine.
Taarifa
ya kundi hilo linalozijumuisha nchi za Marekani, Canada, Ujerumani, Ufaransa,
Uingereza, Japan na Italia imeitaka Moscow kuacha kile ilichokitaja kuwa ni
'kuvuruga hali ya ndani ya Ukraine' au wataiwekea vikwazo zaidi.
Wakati
huo huo Rais Barack Obama wa Marekani imeituhumu Moscow kuwa inatumia 'mbinu
giza' za karne ya 20 nchini Ukraine, na kuahidi kukabiliana na kile alichodai
ni uingiliaji wa Russia huko mashariki mwa Ukraine.
No comments:
Post a Comment