MURSI AWATAKA WAMISRI KUENDELEA NA MAANDAMANO KUIPINGA SERIKALI
MPYA YA NCHI HIYO
Rais halali aliyepinduliwa na jeshi nchini Misri Muhammad
Morsi amewataka wananchi waaendelee kuandamana na kupinga serikali mpya ya nchi
hiyo.
Kupitia ujumbe wake aliotuma kutoka jela, Morsi amewataka
Wamisri waendeleze maandamano ya mapinduzi ya amani dhidi ya serikali
inayoungwa mkono na jeshi akisema kuwa, mapinduzi yatashinda hivi karibuni huko
Misri.
Pia Morsi amekiri kuwa alifanya baadhi ya makosa alipokuwa
madarakani lakini hata hivyo amesema hakuwafanyia khiyana Wamisri na kuahidi
kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi na jinai nchini humo.
Ujumbe huo umetolewa ikiwa ni siku moja baada ya
kuapishwa rasmi Abdul Fattah al Sisi aliyekuwa mkuu wa jeshi wa zamani wa Misri
kuwa rais wa nchi hiyo
Hatua hiyo imefikiwa baada ya tume ya uchaguzi
kutangaza kuwa ameshinda uchaguzi kwa asilimia 96.91
Hata hivyo, uchaguzi huo ulikumbwa na dosari kubwa ya kususiwa
na makundi mengi ya kisiasa ya Misri huku wanachi wakijitokeza kwa kiasi kidogo
sana katika upigaji kura.
SHUKRAN
ReplyDelete