SHEIKH
MUHAMMAD HUSSEIN, MUFTI WA BAYTUL MUQADDAS AMEUONYA UTAWALA WA KIZAYUNI DHIDI
YA KUKIVUNJIA HESHIMA KIBLA CHA KWANZA CHA WAISLAMU (MASJID AL-AQSWA)
Sheikh
Muhammad Hussein, Mufti wa Baytul Muqaddas ameuonya utawala wa Kizayuni kwa
kuendelea kuushambulia na kuuvunjia heshima msikiti wa kihistoria wa al Aqsa
ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Mufti
huyo wa Baytul Muqaddas ametoa tamko akiutaka ulimwengu wa Kiarabu na ulimwengu
wa Kiislamu kusimama imara kupambana na jinai za kila leo za utawala wa
Kizayuni wa Israel na kulinda haki za taifa la Palestina na maeneo matakatifu.
Amesema,
viongozi wa Israel wanapuuza vitendo viovu vinavyofanywa na walowezi wa
Kizayuni katika msikiti wa al Aqsa, huku wanajeshi wa utawala huo dhalimu
wakiendelea kuwazuia Wapalestina wasiotimiza miaka 50 kuingia hata katika eneo
tu la msikiti huo.
Ni hivi
majuzi tu, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walipouzingira msikiti huo kwa
madai ya kipuuzi na kupiga marufuku ya kuingia na kutoka eneo hilo, ili
kuwazuia Wapalestina kuingia sehemu hiyo takatifu.
Baada ya
wanajeshi wa Israel kuuzingira msikiti wa al Aqsa, walowezi wa Kizayuni
wakisaidiwa na wanajeshi hao, waliuvamia msikiti huo na kulivunjia heshima eneo
hilo takatifu.
Lengo la
Wazayuni la kuuvamia mara kwa mara na kuchimba mashimo na mahandaki pambizoni
mwa msikiti huo, ni kukiharibu kikamilifu kibla hicho cha kwanza cha Waislamu
eneo ambalo pia lina historia kongwe.
Kwa
mujibu wa takwimu za taasisi ya Palestina ya Wakfu na Turathi za al Aqsa, tangu
mwanzoni mwa mwaka huu wa 2014 hadi hivi sasa, Wazayuni 6311 wenye misimamo
mikali wameuvamia msikiti huo na kuuvunjia heshima.
Wazayuni
hao ni pamoja na walowezi wa Kizayuni, majasusi wa Israel pamoja na wanajeshi
wa utawala huo dhalimu.
Mara
nyingi uvamizi wa msikiti wa al Aqsa unafanywa na vikosi maalumu vya Israel na
lengo lake ni kuwatia hofu Wapalestina wanafika eneo hilo kusali.
Taasisi
ya al Aqsa imetoa takwimu hizo kwa kushirikiana na taasisi nyingine
inayojulikana kwa jina la Taasisi ya Uimarishaji wa Msikiti wa al Aqsa na
Matukufu yake.
Taasisi
hizo za Palestina zimeonya kuwa, Wazayuni wamepanga kuendelea na jinai zao
kwenye kibla hicho cha kwanza cha Waislamu, hivyo hatua za haraka zinatakiwa
ili kuzuia jinai hizo.
Kwa
upande wake Sheikh Abdul Adhim, Mkuu wa Baraza la Wakfu wa Kiislamu ambaye ni
miongoni mwa viongozi waandamizi wa masuala ya uimarishaji wa Msikiti wa al
Aqsa ameashiria uvamizi wa hivi karibuni wa walowezi wa Kizayuni katika msikiti
huo na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka za kuliokoa eneo
hilo takatifu la kihistoria.
Jinai za
Wazayuni dhidi ya Wapalestina na dhidi ya matukufu ya Kiislamu zinatendeka huku
madola ya Magharibi yakiendelea kuunga mkono kwa kila namna utawala wa Kizayuni
wa Israel.
Hata
hivyo fikra za walio wengi duniani zinazidi kuamka, na kadiri Wazayuni
wanavyofanya jinai na dhulma dhidi ya Wapalestina, ndivyo hasira za walimwengu
zinavyozidi kuongezeka dhidi ya utawala huo pandikizi.
No comments:
Post a Comment