Monday, June 9, 2014

HOJA NA MAONI YETU WAISLAMU JUU YA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA. ISIKHALIFU KITABU CHA ALLAH KWA KUZUIA IBADA ZA WAISLAMU





Sehemu ya 1.
1.     Kwamba Katiba iliyopo haitambui kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na uhalali wa mamlaka ya Mwenyezi Mungu
Katiba mpya itambuwe kuwepo kwa Mwenyezi Mungu na Mamlaka yake juu ya Wanaadamu (kwa mnasaba huu, wananchi wa Tanzania)
2.     Kwamba Katiba iliyopo haitambui uhalali wa Sheria za Mwenyezi Mungu. Hii inajidhihirisha kwa kauli ya serikali kutokuwa na dini.
Katiba mpya iweke wazi kutambua kwake uhalali wa sheria za Mwenyezi Mungu na kuziheshimu. Maana ya serikali kutokuwa na dini iainishwe na kuwekwa wazi kikatiba.
3.     Kwamba Katiba iliyopo inamlazimisha mtu kufuata sheria zote hata kama zinakwenda kinyume na imani ya dini ya raia husika.
Katiba mpya isimlazimishe mtu kufuata taratibu au sheria ambazo inakwenda kinyume na imani yake na hivyo kupelekea kuvunja sheria za dini yake.
4.     Kwamba Katiba iliyopo haitoi tafsiri yakinifu juu ya maana ya ibada na dini.
Tafsiri sahihi ya maneno dini na ibada ni muhimu ili kuzuia bughudha kwa wananchi wanapokuwa katika matendo ya dini na ibada.
5.     Katiba itoe tafsiri yakinifu ya ibada na dini kwa mujibu wa tafsiri ya dini husika. Kwamba Katiba iliyopo inatenganisha mamlaka ya nchi na mamlaka ya dini. Huu ni mfumo Kristo.
Katiba mpya iruhusu kuchanganya mamlaka ya nchi na ya dini. Mfano uwepo wa Mahakama ya Kadhi itakayoendeshwa kwa hazina ya serikali.
6.     Kwamba Katiba iliyopo imetoa tafsiri potofu ya neno HALALI. Kwa mfano neno rizki halali linajumuisha mathalani hata rizki ipatikanayo kwa kuuza pombe na kucheza bahati nasibu ni halali
Katiba mpya itoe tafsiri sahihi ya neno HALALI kwa mujibu wa imani ya dini na tafsiri hiyo iwe ni yenye kukubalika kiutendaji na katika mahusiano baina ya mwananchi wa dini husika na wananchi wengine nje ya dini husika.
7.     Kwamba Katiba iliyopo haiilazimishi serikali kuitambua siku ya Ijumaa kama siku rasmi ya ibada kwa Waislamu. Hii inasababisha usumbufu mkubwa kwa Waislamu kutekeleza ibada hii hususan wafanyakazi na wanafunzi.
Katiba mpya itambue na kuipa heshima siku ya Ijumaa kuwa ni siku maalum ya ibada kwa Waislamu. Hivyo shughuli zote za serikali zisimamishwe wakati wa kutekelezwa ibada hiyo.
8.     Kwamba Katiba iliyopo haitambui kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi. Hii imepelekea Waislamu kutohukumiana kwa sheria za Kiislamu ambayo ni sehemu ya ibada kwao na vile vile kukosekana kwa msimamizi wa haki inapotokea mzozo baina ya Waislamu.
Katiba mpya iruhusu na itambue uwepo wa mahakama za kadhi zitazoendeshwa chini ya usimamizi wa Kadhi Mkuu na Naibu Kadhi Mkuu wataokao chaguliwa na Waislamu kwa kuzingatia sifa za kielimu katika fani ya sheria ya Kiislamu na kutambuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
9.     Kwamba Kutokana na Katiba iliyopo kutokutambua mahakama ya kadhi ajira rasmi za makadhi hazipo.
Katiba mpya itambue uwepo wa tume ya ushauri wa uteuzi wa makadhi na ajira ya makadhi kwa mahakama za kadhi Tanzania ambayo kikatiba itaitwa Tume ya Utumishi ya Mahakama ya Kadhi.
Tume hii itachaguliwa na Waislamu. Wajumbe wa Tume hiyo watakuwa wafuatao:
1. Kadhi Mkuu ambaye atakuwa mwenyekiti kutoka bara au visiwani;
2. Naibu Kadhi Mkuu ambaye atakuwa naibu Mwenyekiti kutoka bara au Visiwani;
3. Kadhi mmoja wa Mahakama ya Kadhi ya Rufaa atakayechaguliwa na Waislamu;
4. Wajumbe watatu kutoka mahakama ya kadhi.
10.                        Kwamba suala la kugharimia uendeshaji wa mahakama za kadhi linapaswa liwe jukumu la serikali kupitia mfuko wa hazina ya serikali. Hii kwa sababu Waislamu ni sehemu ya walipa kodi. Kama walivyo raia wengine, wanastahili kufaidika kutokana na kodi wanazolipa.
Katiba mpya iilazimishe serikali kugharimia gharama za kuendesha mahakama za kadhi na gharama za watumishi wote kutoka kwenye mfuko wa hazina ya serikali.
11.                        Kwamba Mahakama ya Kadhi haipaswi kuingiliwa na mahakama ya aina yoyote isiyohukumu kwa sheria ya Kiislamu. Kwamba upo umuhimu wa kuundwa kwa Mahakama ya Rufaa ili kusikiliza kesi za rufaa kutoka kwenye mahakama ya kadhi.
Katiba mpya itambuwe uwepo wa Mahakama ya Rufaa ya Kiislamu.
Kwamba Waislamu kwa Katiba mpya itambue haki ya
12.                        Sheria zilizopo wanakwazika katika kutekeleza dini yao kikamilifu. Inawawia vigumu kutekeleza sheria kwa mnasaba wa dini yao. Kufuata sheria za Kiislamu ni sehemu ya dini na ibada ya lazima kwa Muislamu, haki ambayo katiba iliyopo imetoa uhuru. Waislamu kutekeleza nakufuata sheria ya Kiislamu katika ukamilifu wake. Katika sehemu zenye Waislamu wengi sheria ya Kiislamu ifuatwe katika ukamilifu wake. Kila Muislamu katika maeneo haya atalazimika kuhukumiwa kwa sheria za Kiislamu. Katika maeneo yenye Waislamu wachache mahakama za kadhi ziwahukumu Waislamu katika sheria zote za Kiislamu isipokuwa za jinai.
13.                         Kwamba Katiba iliyopo haitoi muongozo juu ya ushirikiano baina ya serikali na dini au madhehebu ya dini, hali iliyopelekea kuwepo kwa malalamiko ya kuwepo kwa upendeleo maalum unaoneemesha Ukristo (hususan Ukatoliki) hususan katika sekta ya elimu na afya kwa kutumia hazina ya taifa. Mathalani kwa kupitia mkataba wa ufahamiano [MoU] baina ya serikali na kanisa serikali hutenga mamilioni ya fedha za umma kila mwaka kunufaisha mipango ya afya na elimu ya kanisa.
Katiba mpya iweke uthibiti wa matumizi ya fedha za umma kwa utaratibu wa upendeleo wa madhehebu ya dini yoyote ama kinyemela au kwa njia ya urasimishaji kupitia mikataba au makubaliano.

No comments:

Post a Comment