TWAHARA
NINI MAANA YA TWAHARA?
KILUGHA.
Ni usafi na kumalizana na uchafu au
takataka za kihisia kama vile najisi kutokana na mkojo au kinginecho, na uchafu
wa kidhahania kamakasoro (mapungufu) na maasi.
KISHERIA.
Ni kuondosha kile chenye kuzuia swala
kutokana na hadathi au najisi kwa kutumia maji (au kinginecho) au kuondosha
hukumu yake kwa mchanga.
HUKMU YA TWAHARA
Twahara ni jambo la wajibu ikiwa
mtu atakumbuka na ataweza. Dalili ni kauli yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Allah
anasema:
((وَثِيَابَكَ
فَطَهِّرْ))
«Na nguo zako zitwaharishe»
Aidha anasema
(Subhaanahu wa Ta'ala):
((أَن
طَهِّرَا بَيْتِيَ لِلطَّائِفِينَ وَالْعَاكِفِينَ وَالرُّكَّعِ السُّجُودِ))
«Ya kwamba
itakaseni Nyumba Yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu na wanaojitenga humo
kwa ibada, na wanaoinama na kusujudu»
Ama kujitwaharisha na hadathi, hilo
ni lazima ili kuruhusika kuswali, kwa kauli yake Mtume (Swalla Allahu 'alayhi
wa aalihi wa sallam)
(( لا تقبل صلاة
بغير طهور))
((Swalah haikubaliwi bila ya wudhuu))
UMUHIMU WA TWAHARA:
1. Ni sharti ya kusihi kwa swala ya
mja. Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((لا تقبل
صلاة من أحدث حتى يتوضأ))
2. Ni kujipamba na sifa ya kuwa kipenzi cha Allah
(Subhaanahu wa Ta'ala). Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amesema:
ُ
((إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ))
Aidha, Allah (Subhaanahu wa Ta'ala)
anasema:
((فِيهِ
رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُواْ وَاللّهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ))
3. Ni kinga kutokana na adhabu za
kaburi. Imepokelewa na Ibn ‘Abbaas akisema: Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa
aalihi wa sallam) alipita kwenye makaburi mawili akasema:
((إنهما يعذبان
وما يعذبان في كبير أما هذا فكان لا يستنزه من
بوله))
((Hakika wao (maiti) wanaadhibiwa,
na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. Ama huyu, alikuwa hajitakasi na mkojo wake….))
AINA ZA TWAHARA
Maulamaa wanaigawanya Twahara ya
kisheria katika vigawanyo viwili:
1.
TWAHARA
YA KIHAKIKA: Nayo ni Twahara ya kuondosha
najisi. Hii inakuwa katika mwili, nguo na mahala.
2.
TWAHARA
YA KIHUKUMU: Ni Twahara kutokana na hadathi, nayo inahusiana
na mwili. Aidha Maulamaa wameigawanya aina hii ya twahara katika hali kuu tatu
(3)
(a)
TWAHARA KUBWA,
nayo ni kuoga
(b)
TWAHARA NDOGO, nayo
ni kutawadha
(c)
TWAHARA YA KATI NA KATI. Nayo ni badala ya viwili hivyo
vinaposhindikana, ambayo ni kutayamamu.
No comments:
Post a Comment