Polisi
ya Sudan imemtia mbaroni kiongozi mwingine wa upinzani nchini humo. Ibrahim
al-Sheikh
Mkuu
huyo wa chama cha Kongresi ya Sudan, ametiwa mbaroni huko katika jimbo la
Kordofan Magharibi, nchini humo.
Ibrahim
amekamatwa na polisi ya Sudan kwa tuhuma za kutoheshimu katiba, kueneza
propaganda za uongo na kutishia usalama wa taifa.
Katibu
wa chama hicho, Abdelqayum Awad amesema kuwa, ikiwa tuhuma anazotuhumiwa
Ibrahim zitathibiti dhidi yake, basi kuna uwezekano wa kuhukumiwa adhabu ya
kifo.
Itakumbukwa
kuwa wiki tatu zilizopita, maafisa wa usalama wa nchi hiyo, walimtia mbaroni
Sadiq al-Mahdi, mkuu wa chama cha Umma aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Sudan kwa
tuhuma za uchochezi dhidi ya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir.
Suala
hilo lilipelekea wafuasi wa kiongozi huyo kuandamana siku ya Ijumaa
wakiishinikiza serikali ya Khartoum kumuachilia huru kiongozi wao huyo.
No comments:
Post a Comment