Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imetoa tamko na kusema
kuwa itaendeleza mapambano dhidi ya serikali ya Rais mpya wa nchi hiyo,
Abdul-Fattah al-Sisi hadi pale demokrasia halisi itakaporejea katika nchi hiyo.
Tamko la Ikhwan limekuja ikiwa ni majibu dhidi ya matamshi ya
Rais al-Sisi ambaye amesema hapo jana kuwa serikali yake itaendeleza mapambano
dhidi ya makundi ya kigaidi.
Ingawa rais huyo mpya hakulitaja kundi la Ikhwanul Mislimin
lakini ni wazi kwamba matamshi yake yalimaanisha kundi hilo kwani serikali ya Misri
inaliona kundi hilo kuwa ni kundi la kigaidi.
Taarifa ya Ikhwanul Muslimin imesema walioko madarakani kwa
sasa ni wezi wa kisiasa walioteka nyara mapinduzi ya wananchi ya mwaka 2011.
Harakati hiyo imewataka Wamisri kuendeleza maandamano dhidi
ya rais mpya kwa lengo la kutetea heshima, demokrasia na adhama ya taifa lao.
No comments:
Post a Comment