Idara ya kupambana na ugaidi nchini Iraq imethibitisha kuuawa mufti
wa kundi la Dola la Kiislamu la Iraq na Sham kwa kifupi Daesh huko mjini Tikrit
nchini humo.
Kwa mujibu wa idara hiyo, mufti huyo wa kundi hilo linalosadikiwa
kuwa ni la kigaidi Swaqru an-Naswir, ameuawa katika operesheni ya jeshi la Iraq
iliyofanikiwa katika mji huo.
Habari zinasema kuwa, operesheni hiyo imefanyika kwa kutegemea
habari za kiintelijensia katika mji huo.
Aidha imesadikiwa kuwa, katika operesheni hizo, zaidi ya wanamgambo
150 wa kundi hilo wameuawa na kujeruhiwa mjini hapo.
Jeshi la Iraq kwa kutumia ndege za kivita lilililenga mkusanyiko
mkubwa wa kundi hilo na kuwawa wengi kati yao.
Aidha jeshi la Iraq pia limefanikiwa kuuangamiza msafara wa magari
ya kundi hilo yapatayo 200 uliokuwa ukielekea mji wa Samarra.
Hii ni katika hali ambayo, Nour al Maliki Waziri Mkuu wa Iraq
amelipa amri jeshi la nchi hiyo kuisafisha miji yote ya Iraq kutokana na uepo
wa kundi la Daesh.
Kwengineko sheikh mkubwa wa Kisuni amelitaja kundi la Daesh kuwa ni
kundi lililopotea na kwamba halina uhusiano wowote na dhehebu la Kisuni.
Sheikh Muhammad Amin mmoja wa wajumbe wa Jumuiya ya Maulama wa Iraq
ameyasema hayo kupitia kanali ya televisheni ya Sumaria News na kusema kuwa,
Iraq inakabiliwa na hujuma za matakfiri ambao wanatekeleza ajenda za mabwana
zao kwa lengo la kuigeuza Iraq kuwa kichaka cha ugaidi.
No comments:
Post a Comment