Waumini wa
dini ya kiislamu nchini wametakiwa kuwa na subra hasa katika kipindi hichi
kigumu ambapo nguvu za madui dhidi ya waislamu zimeelekezwa kichafua dini hiyo
ya amani, upendo na utulivu.
Kauli hiyo
imetolewa na sheikh Mohammed Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari
kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea kujitokeza katika nchi za kiislamu na
maeneo mbalimbali ya waislamu ikiwemo kisiwa cha Zanzibar.
Amesema,
waislaam wamekabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa maadui zao ikiwa ni pamoja
na maadui hao kupanga njama mbalimbali za kutaka kubomoa msingi wa uislamu na
kuwapaka matope waislamu hao.
Hayo yamejiri
kufuatia matukio ya kuuwawa kwa masheikh na viongozi mbalimbali wa kidini ndani
na nje ya nchi, likiwemo tukio la mripuko wa bomu lililosababisha kuuwawa kwa
muhadhiri mmoja huko Zanzibar.
Hata hivyo
uchunguzi unaendelea kufuatia tukio hilo, huku Jeshi la Polisi Zanzibar likisema
kuwa bado halijabaini mtu yoyote au kundi lolote kuhusika na uripuaji wa Bomu katika eneo la darajani huko Zanzibar.
RPC Mkoa
wa Mjini Maghar, Mkadam Khamis wakakati akizungumza kupitia simu yake ya
mkononi na baadhi ya vyombo vya habari amesema, katika tukio hilo mtu mmoja
amefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya kutokea mripuko huo wa
bomu.
Amesema kulionekana
kutokea kwa taharuki wakati waumini wa Dini ya kiislamu walipokuwa wanatoka
msikitini Darajani ambapo kulikuwa na mawaidha baada ya kumalizika kwa sala ya
Ishaa.
Akibainisha
kutokea kwa tukio hilo RPC huyo ,amesema kwamba watu waliokuwa ndani ya gari
ndogo aina ya Vits walirusha bomu hilo na kukimbia kusiko julikana wakati
waumini wa Dini ya kiislamu walipokuwa wanatoka msikitini.
Hadi
sasa Jeshi la Polisi bado halijabaini iwapo bomu hilo ni lakutengeneza kwa
kutumia baruti au ni bomu lenyewe ambalo limetengezwa kwa njia ya kitaalamu.
Ameeleza
kuwa aliefariki katika tukio hilo ni Khatibu Mkumbiladuha (26) mkaazi wa Mkoa
wa Tanga ambae alikuwa miongoni mwa wahadhir waliofika msikitini hapo.
Aidha
RPC Mkadam amewataka wananchi wa Zanzibar kuwa watulivu katika kipindi hichi
huku wakiliacha Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini
wahusika wa tukio hilo na hatimae kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Katika
kipindi cha hivi karibuni Zanzibar imekuwa akikubwa na matukio mbali mbali ya
uchafuzi wa amani ikiwa ni pamoja na kuuwawa kwa viongozi mbalimbali wa kidini jambo
linalotishia amani mjini humo.
Wachambuzi
wa mambo wameendelea kudai kuwa hali hiyo inaonekana ni njama za makusudi za
kutaka kukichafua kitovu hicho cha uislamu kwa maslahi yao binafsi.
No comments:
Post a Comment