Mshauri wa mufti nchini Misri amelitaja kundi linalojiita kwa jina
la Dola la Kiislamu la Iraq na Sham kwa kifupi DAESH kuwa ni kundi lenye
fikra potofu na kwamba ni haramu kwa mtu yeyote kujiunga na kundi hilo.
Ibrahim Najmi amesema kuwa, kundi hilo licha ya kuwa na misimamo
isiyokubalika na Uislamu, limewahadaa vijana wengi kwa kauli ya eti Dola la
Kiislamu, katika hali ambayo vitendo vyake vinafanyika kwa lengo la kuuchafua
Uislamu, kuharibu nchi na kumwaga damu za watu.
Ibrahim ameyasema hayo katika kikao cha waandishi wa habari katika
ofisi ya Kiislamu ya DARUL-FATWA mjini Cairo, Msri.
Aidha amesisitiza kwamba, Watu wanapasa kuchukua hatua madhubuti za
kukabiliana na fikra za makundi yenye kuuchafulia jina a Uislamu mithili ya DAESH
na mengineyo ambayo yanatekeleza vitendo vya ukatili kote duniani.
Amemalizia kwa kusema kwamba, vitendo vya kundi la DAESH yakiwemo
mauaji na uharibifu huko nchini Iraq, Syria na katika nchi nyingine,
vinafanyika kwa maslahi ya maadui wa umma wa Kiislamu hasa kwa kuzingatia
kwamba uharibifu na mauaji hayo yanafanyika katika nchi za Kiislamu kwa lengo
la kuwadhuru Waislamu.
No comments:
Post a Comment