Tuesday, June 17, 2014

MWANDISHI WA HABARI WA TELEVISHENI YA AL-JAREERA, ABDULLAH ELSHAMY AAMURIWA KUACHIWA HURU



Mwendesha mashtaka mkuu nchini Misri ameamuru kuachiliwa huru kwa mwandishi wa habari wa televisheni ya Al-Jazeera ambaye amekuwa akifanya mgomo wa kususia kula chakula kwa zaidi ya miezi minne ili kulalamikia kuendelea kuzuiliwa kwake bila kufunguliwa mashitaka. 


Ofisi ya mwendesha mashtaka imesema Adbullah Elshamy mwenye umri wa miaka 26 na wenzake 12 wataachiliwa huru ikitaja "sababu za kiafya". 

Hata hivyo, taarifa hiyo imemtaja Elshamy pekee na hakuna wanahabari wengine watakaoachiliwa. 

Amri hiyo ya kumwachia Elshamy imekuja katika siku ambayo jaji anayeongoza kesi ya waandishi wa habari watatu wa Aljazeera amesema kuwa mahakama itatoa uamuzi wake mnamo Juni 23, ikiwa ni miezi mitano baada ya kesi hiyo kufunguliwa.

No comments:

Post a Comment