Friday, June 27, 2014

TULIYOKUKUSANYIA KUHUSU MUANDAMO WA MWEZI WA RAMADHANI 2014

NA MWANDISHI WAKO UST. MUBARAKA

Waislamu nchini Tanzania wanatarajia kuungana na waislamu wengine duniani kote kuanza mfungo wa ramadhani unaotarajiwa kuanza siku ya Jumaapili tarehe 29 June 2014

Hata hivyo, miongoni mwa waislamu hao wameonekana kuanza kisimamo cha swala ya tarawehe usiku huu kuashiria kuungana na waislamu wenzao wa Yemen  ambao wameanza rasmi kuupokea mwezi mtukufu wa ramadhani hii leo.

 Yemen imekuwa nchi ya pekee hadi sasa kutangaza kuanza kwa mfungo wa ramadhani, huku Umoja wa Mataifa ya Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia sambamba na nchi nyingi za kiislamu zikitangaza kutokuonekanwa kwa mwezi mwandamo na hivyo kesho kuwa ni shaaban 30.
 
Nchi nyingine ambazo zimetangaza kutokuonekanwa kwa mwezi na kwamba kesho ni tarehe 30 shaaban ni pomoja na Kuwait, Qatar, Oman, Egypt, Jordan, Bahrain, Palestina na Indonesia. 

Msimamizi wa Msikiti Mitukufu ya Makkah na Maddina, king Abdullah Bin Abdullaziz amemtumia salaamu za rambirambi raisi wa Yemen Abdrabbon Mansour huku akimtakia mfun go mwema wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Kwa upande wa kamati ya mwezi ya umoja wa mataifa ya kiarabu (UAE) imetangaza leo ijumaa jioni kuwa mwezi mtukufu wa ramadhani utaanza siku ya jumapili. 

Mahakama ya sheria nchini Saudi Arabia imethibitisha kuwa mwezi haukuonekana na kwamba kesho itakuwa ni siku ya mwisho ya mwezi wa shaabani 30  na hivyo ramadhani itaanza jumapili Juni 29.

Kamati ya mwezi ya mataifa hayo imeeleza kuwa wameanza kufuatilia mwandamo wa mwezi mapema tu baada ya swala ya Magharibi katika mabonde mawili makubwa nchini humo.

Ikumbukwe kuwa nchi nyingi tu za kiarabu, Europe, amerika na Canada huanza mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kufuata Saudi Arabia.








Baadhi ya vyanzo vya habari vya utafiti wa mwandamo wa mwezi vimeeleza kuwa, mwezi mwandamo wa ramadhani umezaliwa leo Ijumaa Juni 2014, muda wa saa 12 : 18 (Local time) na jua limezama kwa dakika 07 na 12 huku mwezi ukiwa na masaa 07 na dakika 4 na kwa hali hiyo mwezi ulikuwa upo chini kiasi kwamba nivigumu kwa mwezi mwandamo kuonekana.

Kwa upande wa chama cha Harakat Al-Shabab Al Mujahideen nchini Somalia kupitia Radio Al Andalus kimetangaza kuwa siku ya kesho si Ramadhan na hivyo kesho kuwa siku ya mwisho wa Sha'aban. 

Watumishi wa ofisi ya haki na Sheria ya Harakat Al-Shabab Al Mujahideen imesema hayo baada ya kufanya juhudi ya kutafuta mwandamo wa mwezi wa Ramadhaan na kutangaza kuwa siku ya Jumapili ndio Ramadhani Mosi.


Radio Al Andalus inayozungumza kwa niaba ya Harakat Al-Shabab Al Mujahideen nayo imetangaza kuwa siku ya kesho itakuwa Sha'aban 30 1435.

Aidha imesema kuwa, maeneo yote ya Wilaya za Kislaam Kusini na katikati mwa Ardhi ya Somalia hakuna sehemu iliyoonekana mwandamo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhaan








No comments:

Post a Comment