Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesisitiza juu
ya ulazima wa kufunguliwa mashtaka wale wote waliohusika kwenye mauaji ya
waislamu wasio na hatia na kutenda jinai mbalimbali nchini humo.
Isabelle Gaudeuille amesema kuwa, mwishoni mwa mwezi
uliopita, serikali ya Bangui iliiomba Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ifanye
uchunguzi kuhusiana na jinai zilizofanywa na kundi la kigaidi la kikiristo la
Anti balaka nchini humo.
Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesisitiza
kwamba kuna udharura mkubwa kwa mahakama hiyo ya kimataifa kuanza kuchunguza
haraka jinai zilizofanyika nchini humo na kufunguliwa mashtaka watuhumiwa wote
wa jinai hizo.
Wakati huohuo, makundi mbalimbali nchini Jamhuri ya Afrika ya
Kati yameanza mazungumzo yenye lengo la kurejesha amani na utulivu nchini humo.
Taarifa zinasema kuwa, wawakilishi kutoka makundi ya kiraia,
harakati za kisiasa, viongozi wa kidini, wachumi na wawakilishi wa jeshi wameanza
kikao cha faragha cha siku tatu kinachojadili hali ya kiusalama nchini humo.
Hayo yanakuja huku ikiwa maelfu ya waislamu tayari wamekwisha
kuyahama maeneo yao na kugeuka wakimbizi na wengine wengi kuuwawa kinyama na
kikatili huku majumba yao yakibomolewa mali zao kuteketezwa na miskiti kuvunjwa
vunjwa na mingine kugeuzwa majumba ya starehe.
No comments:
Post a Comment