Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya
Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua
hatua za dharura ili kukomesha mashambulizi ya utawala ghasibu wa Israel katika
eneo la ukanda wa Gaza.
Khalid Mash’al ametoa wito huo wakati alipozungumza
kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Ahmet Davotoglu.
Kwenye mazungumzo hayo, Mash’al amesema nchi za
Kiislamu kama vile Uturuki na nyinginezo Mashariki ya Kati zinapaswa kusimama
imara na kupinga kivitendo hujuma za Wazayuni dhidi ya raia wasio na hatia
katika ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Utawala wa Kizayuni wa Israel kwa siku kadhaa
sasa umekuwa ukiendesha mashambulizi dhidi ya maeneo mbalimbali ya Palestina
hususan ukanda wa Gaza kwa kisingizio cha kuwatafuta vijana watatu wa Kizayuni
waliotoweka.
Kwenye hujuma hizo, Wapalestina watatu wameuawa
shahidi na wengine kadhaa wamejeruhiwa
No comments:
Post a Comment