Tuesday, July 1, 2014

KOPLO MUASI WA MAREKANI MBARONI




Koplo katika jeshi  la Marekani  ambaye  alitangazwa  kuwa ameasi  na  kutoroka  jeshi  miaka  10 iliyopita baada  ya kutoweka  nchini  Iraq katika  mazingira  yasiyoeleweka amepatikana  na  yuko  mikononi mwa  jeshi  la  Marekani na atakabiliwa  na  mashtaka.


Koplo Wassef Ali Hassoun , mwenye  umri  wa  miaka  34, amejisalimisha  na amepelekwa  kutoka  katika  eneo  ambalo  halikutajwa katika   mashariki  ya  kati   na  kupelekwa  Virginia nchini Marekani.


Kwa  mujibu wa msemaji  katika  makao  makuu  ya  jeshi la  majini  katika  wizara  ya  ulinzi kapteni Eric Flanagan amesema, koplo huyo anatarajiwa  kupelekwa  katika  kituo  chake  cha mwanzo  cha  Camp Lejeune  kaskazini  mwa  Caroline.


Meja jenerali Raymond Fox, kamanda  wa  kikosi  cha  pili katika  kambi  ya  Lejeune, ataamua katika  muda  wa  siku kadhaa jinsi  ya  kuendeshwa  kwa  kesi  hiyo, ambayo itakuwa  na  maana ya  mahakama  ya  kijeshi


No comments:

Post a Comment