Seikali ya Tanzania imelaani mauaji
yanayofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wakazi wasio na
ulinzi wa Ukanda wa Gaza, huko Palestina.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa
nchi hiyo, Bernard Membe ambapo pamoja na mambo mengine ameitaka jamii ya
Kimataifa hususan Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka kuzuia jinai hizo
za Wazayuni katika eneo hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania amekosoa pia
kimya cha walimwengu mbele ya jinai hizo ambazo zinakinzana na sheria zote za
kimataifa.
Hiyo ni kauli ya kwanza kutolewa na nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tangu kulipoanza mashambulizi ya
utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza siku nane zilizopita.
No comments:
Post a Comment