Wednesday, July 2, 2014

MSINGI WA MWANAFUNZI KATIKA KUFIKIA MAFANIKIO.



UNIVERSITY OF DARES SALAAM

MSINGI WA MWANAFUNZI KATIKA KUFIKIA MAFANIKIO.

 

MUBARAKA A.  HAMAD.

 Hakuna kisichowezekana ndani ya wakati maalumu, njia muafaka, na mbinu stahili. Nakala hii ni suluhisho lako wewe ndugu mwanafunzi, kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vikuu, anza sasa uone mafanikio.

MISINGI MIKUU YA KUFAULU KIMASOMO NA KIMAISHA.

1. Kumtegemea Mungu Muumba (Allah (SW))

2. Kufanyakazi Kwa bidii {Hard working}.


MBINU ZA USOMAJI {LEARNING TECHNIQUES}.

1. Maandalizi {preparation}.  

2. Umakini {concentration}


MAANDALIZI {PREPARATION}

Kimsingi mwanafunzi hanabudi kufanya maandalizi kabla ya kuanza kusoma kwake.  Maandalizi yapo ya aina mbili.

(a) Ndani ya darasa                  (b) Nje ya darasa


MAANDALIZI YA DARASANI  {CLASS ROOM PREPARATION}.
Mwanafunzi itamlazimu kufanya maandalizi akiwa darasani, Namna gain itamuwezesha  kuyakabili mazingira ya darasani. Maandalizi hayo ni pamoja na.

{a} Kumfahamu Mwalimu {understanding of your teacher}, Mwanafunzi hanabudi kumsoma mwalimu wake nini hasa Mwalimu anahitaji katika kazi zake.

Mwanafunzi asome mgogotezo {emphasis} wa mwalimu katika kazi zake au wakati wa ufundishaji wake.

Mwanafunzi ajaribu kusoma namna ya utungaji wa maswali wa mwalimu wake.

{b} Kufahamu sehemu yako darasani {understanding of your place in the class}, Inambidi Mwanafunzi kufahamu sehemu gani inaweza kumfaa zaidi akiwa darasani. Uzoefu unaonesha wanafunzi waliwo wengi hupenda kukaa sehemu za nyuma au mbali na mwalimu, kutokana na sababu moja au nyengine zikiwemo kukimbia kuulizwa maswali na walimu, au mapenzi tu kwa baadhi ya watu. Mwanafunzi hana budi kujitathimini mwenyewe wapi panamfaa kua sehemu muafaka kwake. Kwa wanafunzi waliwo wadogo kiumri au wafupi darasani wanashauriwa wakae maeneo ya mbele zaidi ili waweze kumsikia na kumuona mwalimu na kile anachokifundisha.

Aidha, baada ya mwanafunzi kuifahamu sehemu yake anashauriwa asiwe ni mwenye kubadilisha badilisha sehemu hio, yaani aifanye sehemu hio kua ni sehemu ya kudumu, Mwanafunzi afahamu kua sehemu yake hiyo pia inamchango mkubwa katika ufahamu wake wa somo husika.

{c}Mahudhurio {attendancy}, Ni msingi mkubwa mno katika uwelewa wa mwanafunzi. Mwanafunzi hanabudi kudumu katika vipindi vyote darasani. Hili litamsaidia kumuweka sawa kiakili  kabla na baada ya kumaliza kusoma .

Pamoja na hilo, Mwanafunzi hanabudi kufika darasani mapema kadri iwezekanavyo, Jambo hili litamsaidia mwanafunzi katika kuiandaa au kuituliza akili yake, na kuiweka tayari kupokea kile atachopewa na mwalimu wake.

{d} Mwanafuzi aingie darasani akiwa na zana {nyenzo} kamili za kujifunzia {equipments of study}. Hizi ni pamoja na madaftari, kalamu na penseli. Hutofautiana baina ya somo moja na jingine.

Kuna wanafunzi wengine hushindwa kuandika au kukopi muhtasari {note} wakati mwalimu akiwa anafundisha, kutokana na uvivu, kujifanya wajanja zaidi, au kuhudhuria darasani bila ya kua na nyenzio husika kuhusu somo hilo. Kinachofanyika kwa wanafunzi hao ni  kutafuta  madaftari ya wanafunzi wengine na kukopia kutoka kwawo.

Uzoefu unaonesha kuwa wanafunzi wa aina hii siku zote mwisho wawo ni  kufeli.

{e} Kuchagua rafiki wa kukaa nae darasani {class mate}.Rafiki unaekaa nae karibu darasani ananafasi kubwa katika kufaulu au kufeli kwa mwanafunzi, Baadhi ya wanafunzi huwa ni watundu na wasumbufu hususan mwalimu akiwa anafundisha darasani. Mwanafunzi anapaswa kutafuta rafiki ataemsaidia kimawazo na sio kumdumaza na kumueka mbali kimawazo wakati mwalimu anafundisha  darasani.

                                                   

UMAKINI {CONCENTRATION}

Mwanafunzi hanabudi kujilazimisha kumfatilia mwalimu kuanzia mwanzo wa somo hadi hatma yake.

Mwanafunzi analazimika kuzishirikisha nyezo zake za hisia zikiwemo ngozi, masikio, pua,macho na mdomo (ulimi).

Pamoja na hilo, mwanafunzi hanabudi kuwa mbali na matumizi ya vifaa kama vile simu, hasa kwa wanafunzi wa ngazi za awali na sekondari.


2. NJE YA DARASA {OUT OF THE CLASS-ROOM}
MARUDIO {REVISSION}.
Mwanafunzi lazima aandae muda maalumu wa kupitia upya kazi au masomo yake. Inashauriwa kwa mwanafunzi kufanya marudio siku hile hile ambayo aliweza kujifunza somo hilo darasani, hii inamsaidia mwanafunzi kukumbuka vyema dhana {concepts} mbali mbali ambazo mwlimu alizifundisha.

Pia, mwanafunzi hanabudi kuheshimu taratibu au mipangilio ya usomaji wake kulingana na ratiba [time table} aliyojiwekea mwenyewe.

Inashauriwa muda wa kujisomea usizidi masaa mawili {2} kwa kitako kimoja.

Nyakati zifuatazo zinapendekezwa zaidi.     

Saa kumi jioni hadi magharibi, Magharibi hadi Ishaa, Baada ya Ishaa hadi saa tano usiku, au saa nane hadi saa kumi usiku, au baada fajri adi saa mbili asubuhi.


SEHEMU NZURI YA KUJISOMEA {GOOD PLACES OF STUDYING}

Wakati mwanafunzi anapotaka kujisomea au kufanya marudio ya masomo yake, azingatiye mambo yafuatayo katika eneo husika.

{a} Hewa {air}   [b} Mwanga {light}     {c} Ghasia {trouble}

Mwanafunzi ajiepushe na kauli NITA….NITA….NITA, bila kuingia katia utendaji. Wanafunzi wengi hujikuta wanaingia katika hali ngumu kutokana na kuendekeza kauli NITA.. NITA…

UMAKINI WAKATI WA KUFANYA MARUDIO  

Mwanafunzi anashauriwa ajisomee katika sehemu iliyo kimya, isiyokua na ghasia na pisha pisha za hapa na pale.

Kinyume na hivyo , Mwanafunzi hanabudi kuhudhurisha viungo vyake vyote vya hisia,kipindi akifanya marudio ya kazi husika.

Pamoja na yote hayo, Mwanafunzi hana budi kuangalia aina gani ya chakula kama yeye ni mwanafunzi. Vyakula vyenye mafuta mengi au sukari nyingi anashauriwa mwanafunzi ajiepushe navyo, au apunguze kuvitumia, badala yake mwanafunzi atumia sana vyakula vya aina ya matunda, ikiwa patakua na uwezekano huo. Hali hii itategemea pia uwezo wa familia yamwanafunzi mwenyewe.


ZINGATIA

1. Mwanafunzi itamlazimu abadilishe mfumo wa usomaji wake pale endapo tu itakaribia kipindi cha mitihani. Mwanafunzi anashauriwa kushiriki katika masomo mchanganyiko {group discussions}, jambo hili litamkumbusha wapi ufahamu wake haukua sahihi, na wapi amefanikiwa katika usomaji wake, vile vile itamsaidia mwanafunzi kumjengea uaminifu {self-confidence} katika masomo yake.

2. Aidha  mwanafunzi anashauriwa kwa kipindi hichi kifupi kutokujishughulisha sana katika kutafuta vitabu mbali mbali na kuanza kujisomea kama kazi kama vile za  fasihi {literatures} na vitabu vya masomo mengine, badala yake ajishughulishe zaidi na kile alichokikusanya katika akili yake na ufupisho {summary} zake.

3. Mwanafunzi azingatie mkao wake kipindi chote cha usomaji wake. Mwanafunzi ajiepushe kusoma ilhali amelala chale, au aina yoyote ile ya ulalaji. Bali anatakiwa akae kitako katika sehemu mzuri, na huku  mgongo wake umenyooka wima.

4. Mwisho kabisa, Mwanafunzi ajiweke mbali na kila aina ya maaswi {evils}, kama vile zinaa {uzinzi},uvutaji wa bangi,na aina zote za vilevi.

 

“PENYE NIA PANA NJIA”
“IN THE WILL THERE IS A WAY”



No comments:

Post a Comment