Tuesday, July 1, 2014

RAISI KIKWETE KUFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA



Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kufungua maonyesho ya kimataifa ya utalii ya Swahili Tourism Expo yatakayofanyika kuanzia Oktoba Mosi hadi 4 mwaka huu.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema hayo wakati akizindua tovuti ya taarifa za maonyesho hayo jijini Dar es Salaam.

Maonyesho hayo yatahusisha kampuni binafsi, taasisi za kiserikali ikiwemo Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), na nchi zote za Afrika Mashariki.

Amesema, hiyo ni fursa ya kuongeza biashara ya kitalii nchini ambapo baada ya hapo Tanzania itapokea watalii zaidi ya milioni mbili kwa kuwa maonesho hayo yataitangaza nchi.

Nae, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB, Balozi Charles Sanga amesema maonesho hayo ni chachu ya kukuza utalii wa ndani.


No comments:

Post a Comment