Wananchi
na wadau mbalimbali nchini wameipongeza Taasisi ya “Al–Madinah” kwa kujumuika
kwa pamoja na zaidi ya watoto 500 walio katika mazingira magumu na mayatima
katika kusherehekea siku kuu ya Eid l fitri.
Watoto
hao kutoka katika vituo mbalimbali jijini Dare s Salaam walipata fursa ya kula
na kufurahi kwa pamoja wakati wa karamu ya chakula cha watoto mayatima
iliyoandaliwa na taasisi ya Almadinah Social Service Trust na kudhaminiwa na
kampuni ya ufuaji wa umeme ya (IPTL).
Mkurugenzi
wa taasisi hiyo Sheikh Ally Mubaraka aliyeandaa tukio hilo amesema, taasisi
hiyo imegundua kuwa mayatima wengi hukumbwa na changamoto nyingi ambazo ni
pamoja na mahitaji ya msingi yakiwemo chakula, makazi na malazi.
Wadau
na wananchi mbalimbali jijini Dare s Salaam wameipongeza taasisi hiyo kwa tukio
hilo la kuweza kuwakumbuka mayatima, na watoto wanaoishi katika mazingira magumu
kwani nao wanapaswa kufurahi kama watoto wengine katika maisha yao.
Aidha,
wameziomba taasisi mbalimbali nchini kuiga mfano huo ili kuwaondolea simanzi na
majonzi watoto hao, ili waweze kuishi katika hali ya furaha na amani kama
watoto wengine.
No comments:
Post a Comment