Sheikh
wa Mkoa wa Singida, Salum Mahami amewaomba wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA) kurejea bungeni na kuwapatia watanzania katiba itakayoendeleza
amani na utulivu uliopo kwa miaka 50 ijayo.
Sheikh
Salum ametoa nasaha hizo wakati akihutubia mamia ya waumini wa dini ya kiislamu
wakati akizungumza na waumini hao katika uwanja wa Namfua mkoani hapo.
Amesema,
UKAWA wasiporejea bungeni na kuendelea na msimamo wao, watakuwa hawaja watendea
haki watanzania.
Amesema,
wananchi wanashauku ya kuona wajumbe wote wamerejea katika meza ya kuijadili
rasimu ya pili ya katiba ili kuwapatia watanzania katiba bora itakayowanufaisha
wananchi wote.
Amesema,
haoni sababu ya wajumbe wa bunge hilo maalumu kuendelea kuendelea kuvutana kwa
hoja ya muundo wa serikali kuwa tatu au mbili kwani wenye haki ya kuamua muundo
gani unawafaa watanzania ni wananchi wenyewe.
No comments:
Post a Comment