Tuesday, July 22, 2014

MAUWAJI GAZA HUENDA YAKAONGEZEKA



Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeelezea wasiwasi wake juu ya kuuongezeka kwa mauwaji ya kinyama katika ukanda wa Gaza.

Kufuatia wasiwasi huo, baraza hilo limeitisha kikao cha dharuira kufuatia ombi la Jordan kutokana na kuongezeka kwa vifo na majeruhi katika ukanda huo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza imeeleza kuwa, jumla ya Waizrail 20 wameuwawa wakiwemo pia askari 18.

Nae, Balozi wa Rwanda ambae pia ni mmoja kati ya wenyeviti wa nchi 15 wa baraza hilo, amesema. kikao hicho hicho kimekuja kwa dhumuni la kukomesha uhasama uliopo kati ya pande hizo.

Aidha ameongeza kuwa wito  huo wa haraka ni kufuatia tukio la kinyama la kuuwawa kwa familia ya wapalestina tisa, wakiwemo watoto saba katika eneo la ukanda wa Gaza.








No comments:

Post a Comment