Tuesday, July 1, 2014

MFANYAKAZI WA NDANI AUWA, ADAI KUCHOSHWA NA MATESO!



Mfanyakazi wandani Valetina Karenge (17) mwenyeji wa Wilaya ya Ukerewe, mkoani Mwanza, anadaiwa kumuua bosi wake, Asha Juma (24) kwa kumchoma kisu sehemu ya juu ya titi la kulia kwa madai ya kuchoshwa na manyanyaso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (SACP), Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Sabasaba, Kata ya Utemini, mkoani Mwanza.

Amesema Asha alikuwa karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida na alikuwa akiishi na mfanyakazi wake huyo wa ndani kwa takribani mwaka mmoja sasa.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, mtuhumiwa huyo amekimbia baada ya bosi wake kufariki dunia, lakini majira ya saa nane alikamatwa akiwa kwenye harakati za kutoroka.

Aidha, amesema, mtuhumiwa huyo anahojiwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi zaidi unaendelea kujua chanzo cha mauaji hayo


No comments:

Post a Comment