Saturday, July 5, 2014

MSOMI MASHUHURI DUNIANI, SHEIKH YUSSUF QARDHAWI APINGA KUNDI LA DAESH KUTANGAZA KHILAFA



Msomi wa Misri mwenye makao yake Qatar Sheikh Yusuf Qardhawi ametangaza kupinga tangazo la kundi la Daesh la kuanzisha kile wanachokiita eti ni 'Khilafa' au utawala wa Kiislamu katika maeneo waliyoyateka Iraq. 

Qardhawi ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu ambaye awali aliunga mkono kundi hilo la Daesh huko Syria lakini sasa amesema Daesh ni tishio kwa madhehebu ya Sunni na kwamba 'Khilafa' iliyoanzishwa ni batili kwa mtazamo wa sheria za Kiislamu. 

Qardhawi ambaye amekuwa mashuhuri kutokana na kupinga misimamo ya mataifa ya kimagharibi na kufikia kumuita kama 'Shekhe wa Fitna' kutokana na uungaji mkono wake kwa makundi yanayodaiwa kuwa niyenye misimamo mikali, amesema  hatua ya 'Abu Bakr Baghdadi' kutangaza kuunda 'Khilafa ya Kiislamu' ni kinyume cha sheria za Kiislamu.

Katika matamshi yake, Qardhawi amesema: "Sisi tuna matumaini kuwa  Ukhalifa utarejea katika nchi za Kiislamu. 

Hatahivyo harakati za kundi linalojiita Dola la Kiislamu Iraq na Sham yaani Daesh zitakuwa na matokeo mabaya katika maisha ya Ahle Sunna nchini Iraq na 'Mapinduzi ya Syria'. 

Ameongeza kuwa, kutangaza kuundwa 'Khilafa ya Kiislamu' ni hatua yenye misimamo mikali yenye lengo la kujipatia umashuhuri tu na wala haitakuwa na msaada wowote kwa Uislamu. 

Amesema cheo cha 'Khalifa wa Kiislamu' si cheo cha kundi maalumu na kwamba Waislamu wote wanapaswa kushirikishwa katika uundwaji dola la Kiislamu.

No comments:

Post a Comment