Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime, mkoani Mara linamshikilia aliyekuwa askari
polisi wa kituo cha Moshi, aliyefufukuzwa kazi mwaka 2012 kwa utovu wa nidhamu
kwa kuingia katika ukumbi wa baa akiwa na silaha.
Mtuhumiwa
huyo anashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya riffle ikiwa na
risasi tano, ambayo ni mali Kampuni ya Ulinzi ya Paroma Security, anayotuhumiwa
kuitumia kufanya uhalifu katika maeneo ya mgodi wa Nyamongo.
Kamanda wa Polisi Tarime, Lazaro Mambosasa, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Kamanda wa Polisi Tarime, Lazaro Mambosasa, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Amesema
mtuhumiwa, alikuwa askari wa jeshi hilo Moshi, mkoani Kilimanjaro, na amekutwa
akiwa na silaha hiyo baada ya kutoroka lindo lake na kwenda nayo katika ukumbi
huo.
Kamanda
Mambosasa amesema kuwa Julai 29, walipata taarifa kutoka kwa raia wema za
kuonekana mtuhumiwa maeneo ya Mtaa wa Magamaga, Kata ya Sabasaba, mjini Tarime
akiwa na silaha hiyo yenye namba 58368 TZCAR 65963 ikiwa na risasi tano.
No comments:
Post a Comment