Waumini
wa dini ya Kiislam nchini wametakiwa kujiandaa kwa ajili ya kujiandikisha upya
katika Daftari la Kudumu la Wapigakura katika zoezi linalotarajiwa kuanza rasmi
Desemba, mwaka huu.
Msemaji
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh Rajabu Katimba, ametoa wito huo katika
Baraza la Idd El-Fitri, lililofanyika katika viwanja vya Mwembeyanga, jijini
Dar es Salaam.
Amesema
ni wajibu wa kila muislamu kujiandikisha katika daftari hilo ili kujiandaa kwa
ajili ya uchaguzi mkuu wa mwakani.
Sheikh
Katimba amesema awali ilidaiwa kuwa vitambulisho vya taifa ndivyo
vitakavyohusika katika upigaji kura, lakini taarifa hiyo hazikuwa za kweli na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) yenyewe imezikanusha.
Nae,
Mwakilishi wa Umoja wa Shule za Kiislamu, Sheikh Hashim Saiboko, amesema bado
ipo dhuluma, ambayo inaendelea kutekelezwa kwa wanafunzi wa dini ya Kiislamu,
hasa katika masomo ya dini.
Amesema
masomo ya dini kwa sasa hayahesabiwi kwa wanafunzi wa kidato cha sita, hali
inayosababisha wengine kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea kutokana na somo
hilo kutoingizwa katika rekodi ya alama
No comments:
Post a Comment