Waislamu wametakiwa kuhuwisha sunna ya Mtume
Muhammad (SAW) kwa kukaa itiqaafu hasa katika kumi la mwisho la mwezi mtukufu
wa ramadhani.
Nasaha hizo zimekuja ikiwa ni masiku machache
tangu waislamu duniani kote kuanza kumi la pili la mwezi Mtukufu wa rammadhan
huku wakisubiria kwa hamu kuanza kwa kumi la mwisho ambalo limahsusi kwa ibada
tukufu ya Itiqaafu.
Sheikh Ibrahim ametoa nasaha hizo mapema leo
hii wakati akizungumza na radio Kheri jijini Dar es Salaam
Amesema, inapaswa ifahamike kuwa itikafu ni
ibada adhimu inayompamba muislamu kubaki katika utukufu wake na nafasi yake
mbele ya Allah tabaraka wataala.
Amesema Mtume (SAW) alilitumia kumi la mwisho
la mwezi mtukufu wa ramadhani, kubaki msikitini akimtaja na kumuelekea allah
(SW) huku akiwahimiza jamaa na maswahaba zake kuiendea sunna hio adhimu.
Aidha amesema ibada hii adhimu pia inafanywa
kwa waislamu wa jinsia zote, wake kwa waume kama ilivyothibiti katika maisha ya
Mtukufu wa darja Muhammad (SAW).
No comments:
Post a Comment