Friday, July 11, 2014

WAHITIMU VYUO VIKUU WAPEWA SOMO



Mkurugenzi wa chuo cha biashara na uchumi (RETCO) mjini Iringa, Lucas Mwakabungu amewataka vijana kujiajiri na kuacha tabia za kukaa vijiweni.


Amesema kuwa vijana wanaohitimu katika vyuo vikuu wanaweza kujiajiri katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili kuimarisha kipato chao.


Akzungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za chuo hicho mjini Iringa Mwakabungu amesema ni ajabu kwa vijana wa sasa kuendelea kuhangaika wakati wamehitimu elimu za shahada za vyuo vikuu.


Amesema vijana hao kwa kutumia elimu walizonazo wanaweza kuimarisha uchumi binafsi ndani na nje ya nchi.


Ameongeza kuwa kwa sasa vijana wanatakiwa kutambua kuwa endapo kila fani waliyosomea watataka serikali iwaajiri inaweza kuishia kuzunguka mitaani na kuendelea kuilaumu serikali badala ya kutumia elimu waliyonayo kujiajiri. 

No comments:

Post a Comment