Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua),
kimemuomba Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kuwawajibisha watendaji
wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kutokana
na kushindwa kuwatetea abiria.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, Mwenyekiti wa Chakua, Hassani Mchanjama, amesema tangu kuanzishwa
kwake, Sumatra imeshindwa kusimamia sheria na kanuni za usafirishaji, kufanya
abiria waibiwe na watoa huduma hizo za usafiri.
Mchanjama amesema wamefikia hatua hiyo baada ya
kubaini mamlaka hivyo imeshindwa kusimamia huduma za usafiri wa abiria, kitendo
kinachowafanya watoaji wa huduma kuamua kutoza nauli wanazotaka kinyume na bei
elekezi ya serikali.
Amesema ushahidi wa abiria kupandishiwa nauli
holela upo na kila mara wanapopata malalamiko kutoka kwa abiria, wamekuwa
wakiiandikia Sumatra barua kuijulisha wizi unaofanyika.
No comments:
Post a Comment