Wanawake wa kiislamu wametakiwa kiutumia siku kuu hii ya Eidil fitri katika kuwaangalia wagonjwa, mayatima, wajane na wale wasiojiweza kwa kuwapatia sadaqa ili kuzidi kuzitakasa swaumu zao.
Wito
huo umetolewa na Imamu msaidizi wa masjid Msufini jijini Dar es Salaam,
Samahatu sheikh Amour Iddi wakati wa khotuba ya swala ya Iddil fitri
iliyoswaliwa msikitini hapo mapema hii leo.
Sheikh
Amour amesema, wanawake hawanabudi kuzitakasa saumu zao kwa sadaka kutokana na
wingi wa kutamka maneno yasiyomazuri bila hata ya kukusudia.
Aidha
ametumia fursa hiyo kuwataka waumini hao kuzihifadhi nafsi zao katika kuelekea
kumuaswi Mola wao mlezi ndani ya siku hii tukufu ya Iddil fitri, kwani kufanya
hivyo kutabatilisha matendo yao ikiwemo ibada tukufu ya Swaumu.
Kwa upande
wake, Imam Mkuu wa masjid Msufini, sheikh Qassim Iddi amewataka waislamu
kufurahia siku ya Iddi kwa kutembelea maeneo matukufu yakiwemo makaburi ili
kupata mazingatio ya siku ya hisabu, jambo ambalo litazidisha uchamungu na
kupambana na nafsi zao.
No comments:
Post a Comment