Neema Luswetula, mkazi wa Katoro wilayani Geita
mkoani Mwanza amejifungua watoto wawili wenye jinsia tofauti wakiwa wamefariki
huku wameungana sehemu ya tumbo na kifua.
Akizungumza katika wodi ya wazazi kituo cha
afya cha Katoro, Mzazi huyo amesema kuwa alifika kituoni hapo Agosti 7 majira
ya saa saba usiku, akiwa na uchungu na ilipofika saa 12:00 alfajiri alijifungua
watoto wawili ingawa kwa bahati mbaya walikuwa wamefariki dunia.
Muuguzi wa zamu katika wodi ya wazazi, Joyce
Michael, amesema kuwa Neema alifika na uchungu na kisha kupelekwa wodi ya
wazazi na kwa bahati mbaya alijifungua watoto wawili wenye kilo 5.1 wakiwa
wameshikana viungo vyao huku wakiwa wamefariki dunia.
Aidha, Muuguzi huyo ameongeza kuwa wakati
akimzalisha Neema, amelazimika kuomba msaada kwa mganga wa zamu, Dk.
Daniel Izengo ili kunusuru uhai wa mama huyo, lakini watoto walikuwa wamefariki
dunia
Nae, Mganga wa zamu, Dk. Izengo, amesema Neema
amejifungua watoto wawili walioungana viungo, na kuongeza kuwa kadi yake ya
kliniki ilimtaka akajifungulie Hospitali ya Wilaya ya Geita.
No comments:
Post a Comment