Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma, Alfred
Msovella, amesema kamwe katiba mpya haiwezi kupatikana bila kuwepo na
maridhiano ya kweli kwani katiba ni mali ya wananchi na siyo mali ya wanasiasa.
Msovella, ameeleza kuwa ili kupata katiba mpya
ambayo ni moyo wa nchi ni lazima pande zote zinazovutana kukaa meza moja kwa
ajili ya kupata muafaka wa kweli.
Mkuu huyo wa mkoa, ametoa kauli hiyo wakati
alipokuwa akizungumza na wazazi, walezi pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi
ya St. Ignatius, wakati wa mahafali ya tano ya darasa la saba yaliyofanyika
shuleni hapo.
Amesema kwa sasa kila kona wimbo unaoimbwa ni
kuhusu mchakato wa vikao vya katiba mpya, ambavyo hata hivyo vinaonekana kuwa
na mgawanyiko kutokana na kutokea kwa makundi ambayo hayakubaliani juu ya
uendeshaji wa mijadala ya kujadili rasimu hiyo.
Awali kamati ya shule hiyo ilikuwa imemwalika
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
Kassimu Majaliwa, ambaye alimkaimisha nafasi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa,
Alfred Msovella
No comments:
Post a Comment