Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba, a amesema si busara kutumia vibaya jina la Rais
Jakaya Kikwete kuzima hoja muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba
amesema hoja hujibiwa kwa hoja wala si kwa kauli ambazo haitasaidia maendeleo
ya taifa.
Amesema kuwa midahalo kuhusu katiba mpya
imefanyika mingi na jamii imeshaelewa lipi lenyemanufaa kwa taifa, hivyo wao
ndio watakaokuwa wamwisho kuamua juu ya mustakbali wa taifa la Tanzania kwa
maslahi ya kizazi hiki na kijacho.
Aidha, Jaji Warioba ameendelea kuwaasihi
wajumbe wa Bunge hilo kutanguliza mbele hoja ya maridhiano ili wakamilishe kazi
waliyopewa ya kuwapatia watanzania katiba yenye maslahi kwa taifa na sio kwa
kikundi cha watu au chama cha siasa.
No comments:
Post a Comment