Kikongwe Athumani Kulaba (80) mkazi wa Chanika
jijini Dar es Salaam, amewashangaza wakazi wa eneo hilo alipobainika kuwa
anakula udongo kama chakula kwa zaidi ya miaka 10.
Kwa mujibu wa kikongwe huyo aliyezungumza kwa
shida, amesema kwa sasa amezoea hali hiyo, licha ya kupewa chakula kutoka kwa
wasamaria wanaofika nyumbani kwake.
Amesema sababu ya kula udongo ni ugumu wa
maisha alionao hasa baada ya kutelekezwa na aliyekuwa mwajiri wake na kutomlipa
fedha zake.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Chanika, Mohamed
Katungi amekiri kupokea taarifa hizo kutoka kwa jirani wa Kulaba.
Amesema baada ya jirani huyo kuona hali ya mzee
inazidi kuwa mbaya, alimtaarifu mjumbe wa eneo hilo John Kanguya ili kumpeleka
kituo cha afya Chanika ambapo amegundulika kuwa na Safura.
No comments:
Post a Comment