Friday, August 8, 2014

LHRC YAMJIA JUU SITTA



Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimtaka Spika wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta, kuwaacha wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wake, kwani kiwanyima uhuru wawo ni kukiuka misingi ya demokrasia na utawala wa kisheria.

Akitoa tamko hilo  mbele ya waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa mchakato wa utungaji wa katiba mpya ya Tanzania, Mkurugenzi wa kituo hicho, Hellen Kijo-Bisimba, amesema wamepatwa na mshtuko mkubwa na kauli za baadhi ya viongozi pamoja na baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuhusina na mchakato huo.

Bisimba, amesema matamko hayo mbalimbali yamekuwa yakiminya uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kutoa maoni, na kwa kiwango kikubwa yanakiuka haki za binadamu nchini kama zinavyolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 na 21(2).

Amesema katika mchakato huo mpaka ulipofikia sasa, aliyekuwa Mwenyekiti waTume ya Mabdiliko ya Katiba wala Rais Jakaya Kikwete, hawapaswi kulaumiwa badala yake wajumbe waangalie nini kitafanikisha mchakato huo

No comments:

Post a Comment