Baraza
la Maadili la Kiislamu Tanzania (Bamakita) limelitaka Bunge Maalumu la Katiba
lijitathmini kama lina ulazima wa kuendelea wakati hakuna uhakika wa kupatikana
kwa theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kupitisha rasimu
ya katiba mpya katika Bunge hilo.
Mwenyekiti
wa Bamakita, Sheikh Athuman Mkambaku, amesema wajumbe wa bunge maalumu la
katiba hawanabudi kuweka mbele maslahi ya taifa kuliko maslahi ya vyama au
kikundi cha watu Fulani.
Shiekh
Mkambaku amesema kitendo cha wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kuendelea kususia vikao vya Bunge hilo si kitendo cha busara kwani msimamo
huo unatia shaka juu ya matarajio mema ya Watanzania ya kupata katiba mpya.
Pia
amewaomba watanzania kuuchukua ushauri
wa Rais Jakaya Kikwete na kwamba, alichokisema katika hotuba yake ni ushauri,
mwongozo na maoni yake kama kiongozi mkuu wa nchi, ambaye ana uwezo huo na
kwamba, siyo lazima kwa wajumbe kufuata maoni yake.
No comments:
Post a Comment