Jeshi la Polisi Zanzibar
leo limemkamata mpigapicha maarufu wakujitegemea anayefanya shooting katika
mihadhara mbali mbali yakiislam na makongamano na mikutano yakisiasa al-ustadh
Salim Khatib.
Akizungumza na waandishi
wa habari visiwani zanzibar mlezi wa harakati ya Jumuiya na Taasisi za kiislam
Zanzibar samahatu sheikh Haji Khamis Hajji amesema, Mpiga picha huyo amekamatwa
mara baada yakumaliza majukumu yake ya kupigapicha katika mkutano wa hadhara wa
chama cha upinzani cha National Reconstruction Alliance
NRA uliofanyika katika viwanja vya komba wapya mjini Zanzibar.
Aidha amiri Hajji
amebainisha kuwa hapo nyuma ndugu Salim aliwahi kuitwa polisi nakuhojiwa
kutokana na harakati zake anazozifanya.
Mpigapicha huyo
anaeishi maeneo ya makondeko wilaya ya magharibi Unguja na anakisiwa kuwa na
umri wa kati ya miaka 35 hadi 40.
No comments:
Post a Comment