Tuesday, August 12, 2014

DRT. SHEIN: ZANZIBAR NI AMANI KARIBUNI KWA UTALII!




Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Alhajj Drt. Aliy mohammed Shein, ameitaka Ujerumani kuekeza visiwani humo na kuleta watalii wengi kufuatia kuimarika kwa amani visiwani humo.

Dkt. Shein ameyasema hayo wakati alopokutana na Balozi mpya wa Ujerumani nchini, Ego Kochanke Ikulu mjini Zanzibar

Amesema uhusiano wa Zanzibar na Ujerumani ulianza muda mrefu tangu karne ya 19, ambayo nchi hiyo ilikua miongoni mwa mataifa machache yaliyoyatambua Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Dkt. Shein ameitaka Ujerumani kuleta watalii wengi visiwani humo kwani sekta hiyo imeweza kuimarika sana kutokana na amani na utulivu wa visiwa hivyo.

Kwa upande wake balozi wa Ujerumani, Ego Kochanke ameipongeza Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu na kuahidi kuzidi kuimarisha uhusiano mzuri kati ya nchi hizo.


No comments:

Post a Comment