Tuesday, August 12, 2014

WATANZANIA WAISHIO NJE YA NCHI WALIA NA URAIA PACHA



Watanzania  wanaoishi Nchi za Nje wamekodi mtaalamu mbobezi wa masuala ya uraia na kuomba ruhusa kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta, ili atoe ufafanuzi kuhusu sura ya tano ya rasimu ya pili ya katiba inayozungumzia masuala ya uraia, ikiwamo uraia pacha.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwapo lwa mtaalamu huyo, ambaye ni Profesa Boneventure Rutinwa, kwenye baadhi ya kamati, Katibu wa Bunge Maalum, Yahaya Khamis  Hamad, amesema wananchi hao wamemwandikia maombi hayo Bwana Sitta.

Hata hivyo, Profesa Rutinwa ameeleleza kuwa, kazi hiyo ilitakiwa kufanyika Alhamisi na Ijumaa, wiki iliyopita lakini kutokana na Ijumaa kuwa sikukuu ya Nane Nane, alilazimika kuiahirisha

Kwa mujibu wa Profesa Rutinwa, ametakiwa kutoa ufafanuzi kwenye eneo hilo ndani ya kamati zote 12, kwa muda wa saa Moja lakini ameweza kuhudumia kamati tatu tu, kutokana na kuwepo uhitaji mkubwa wa ufafanuzi.

No comments:

Post a Comment