Wednesday, August 27, 2014

JK AWANASIHI WAKULIMA MVUMERO



MOROGORO


Raisi Jakaya kikwete amewataka wakulima katika tarafa ya Mgeta wilayani Mvumero kufungasha bidhaa katika vifungasho vyenye ubora ili kuongeza thamani ya mazao.

Amesema mazao ya wakulima wa Tanzania yanaweza kuwa na thamani kubwa katika masoko ya nje iwapo yatakuwa na ubora unaokubalika.

Raisi Kikwete ameyasema hayo wakati akitembelea soko la mazao la Nyandira, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wafanyabiashara.

Amesema ipo haja kwa wakulima kwenda Lushoto kujifunza mbinu mbalimbali wanazotumia wakulima wa huko ili na wawo waweze kutumia mbinu hizo.

Awali, Makamu mwenyekiti wa bodi ya Soko la Nyandira, Odensia Thomas amesema mradi huo wa soko ulianzishwa ili kusaidia wakulima kuuza mazao kwa pamoja kwa nia ya kupambana na harakati za kimaisha.



No comments:

Post a Comment