Wednesday, August 27, 2014

MKAPA AFUNGUKA




Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa, amesema tatizo la mgongano wa maslahi miongoni mwa viongozi na watumishi wa umma ni tatizo ambalo Tanzania inakabiliana nalo hivi sasa.

Kadhalika, amesema licha ya serikali kufanikiwa katika kuhakikisha maadili nchini yanazingatiwa, bado lipo tatizo ambalo limeonekana kutopewa uzito unaostahili.

 
Raisi Mkapa amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya kujadili mapendekezo ya kutungwa kwa sheria mpya ya kudhibiti mgongano wa maslahi miongoni mwa viongozi na watumishi wa umma iliyoshirikisha viongozi kutoka sekta ya umma na binafsi.


Amesema tatizo hilo linajidhihirisha pale wenye mamlaka au watoa maamuzi wanapokuwa na maslahi kwenye jambo Fulani, kutumia madaraka waliyonayo katika kuendeleza maslahi yao binafsi badala ya kutoa kipaumbele kwa maslahi ya umma.

Amesema tatizo hilo la mgongano wa maslahi linahitaji kutazamwa kwa umakini mkubwa na kwamba likifumbiwa macho lina madhara makubwa katika uendeshaji wa serikali.


Naye, Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema ipo haja kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kupewa meno ya kuwawajibisha viongozi wa umma wanaobainika kukiuka maadili ya kazi kama ilivyo kwa taasisi nyingine.



No comments:

Post a Comment