ARUSHA
Waandishi wawili
wa habari wa Kampuni ya New Habari (2006), wamefikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na kosa la kupokea rushwa ya sh.150,000 kutoka
kwa mmiliki na Chuo cha Savana Bridge, kilichopo jijini hapo.
Waandishi hao,
Isack Longwe (28) mkazi wa Tegeta, Tanki bovu na Fredy Okoth (36) mkazi wa
Kimanga Tabata jijini Dar es Salaam, wanadaiwa kushawishi kupatiwa sh. laki
tatu ili waharakishe usajili wa chuo hicho kwenye Baraza la Taifa la Vyuo vya
Ufundi (Nacte).
Wamefikishwa
mahakamani na kusomewa mashtaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa na
Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru),
Vailet Machali mbele ya Hakimu Mkazi, Rose Ngoka.
Amedai kuwa
washtakiwa hao walikamatwa Agosti 16 mwaka huu mchana, baada ya kupokea kiasi
hicho cha fedha ikiwa ni sehemu ya sh. 300,000 walizokuwa wameshawishi
kupatiwa.
Akiwasomea maelezo
ya kosa, Ngoka ameieleza mahakama hiyo kuwa washtakiwa wote kwa pamoja mnamo
Agosti 14 mwaka huu, wakiwa Jiji la Arusha walimshawishi mmiliki ambaye pia ni
Mkuu wa chuo hicho, Mselemu Kombe kuwapatia sh. 300,000, ili wakaharakishe
usajili wake Nacte.
Ngoka alidai kuwa
washitakiwa hao walifanya makosa hayo huku wakijua wao kama waandishi wa
habari hawawezi kufanya shughuli za usajili wa chuo.
No comments:
Post a Comment