DODOMA
Rais Jakaya Kikwete anatarajia kukutana na
viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ili
kuzungumzia mchakato wa Katiba.
Katika mkutano huo, Rais Kikwete atakutaka na
wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao unaundwa na vyama vya
NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF.
Aprili 16, mwaka huu wajumbe wa Ukawa na baadhi
kutoka Kundi la 201, walisusia vikao vya Bunge hilo wakitaka msingi wa
mapendekezo ya Rasimu ya Katiba usibadilishwe, wakipinga uamuzi wa kutaka
kuingiza mfumo wa serikali mbili badala ya tatu zilizopendekezwa katika Rasimu.
TCD inaundwa na vyama vya siasa vyenye
uwakilishi bungeni ambavyo ni CCM, CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi, UDP na TLP, huku
vyama visivyo na uwakilishi bungeni vikiwakilishwa na UPDP kinachoongozwa na
Fahmi Dovutwa.
Kwa nyakati tofauti wenyeviti wenza wa Ukawa,
Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR
Mageuzi), wamesema wako tayari kukutana na Rais, ila msimamo wao ni kutaka
ijadiliwe rasimu iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
No comments:
Post a Comment