Wednesday, August 27, 2014

SERIKALI: SASA ELIMU BURE!



MOROGORO


Rais Jakaya Kikwete amesema serikali inakusudia kufuta karo kwa wanafunzi wa shule za sekondari  za serikali, ili kutoa fursa kwa watoto kusoma bure kuanzia elimu ya msingi, ikiwa ni jitihada za kuinua elimu na kuwapunguzia mzigo wazazi.

Pamoja na kufuta ada kwa shule za sekondari, amesema serikali pia inatengeneza utaratibu maalumu kwa ajili ya shule za msingi na sekondari  zilizopo katika maeneo ya jamii ya wafugaji kwa kujenga mabweni ili kuwawezesha watoto waendelee kusoma hata pale wazazi wao wanapohama kutafuta malisho.

Rais Kikwete amesema hayo wakati akielezea mafanikio ya serikali katika kuinua elimu kuanzia ya awali, msingi, sekondari na elimu ya juu nchini, katika mkutano uliwakutanisha wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, wanafunzi na wananchi wa kata ya Mzumbe, wilayani Mvomero  

Rais Kikwete amesema kufutwa kwa ada hiyo utekelezaji wake upo mbioni ili kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bure,  hatua ambayo itasaidia kuinua kiwango cha elimu nchini.
Kuhusu vyuo vikuu, Rais Kikwete amesema serikali inaendelea na mpango wake wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na kwamba tume iliyoundwa kwa ajili ya kupitia ukusanyaji wa maoni na kutoa ushauri, ripoti yake inafanyiwa kazi ili kuzikabili changamoto hizo.

No comments:

Post a Comment