Wednesday, August 20, 2014

MAAFISA WENGINE WA POLISI WAKAMATWA NCHINI UTURUKI



ANKARA

Maafisa wengine kadhaa  wa  polisi  wamekamatwa  nchini Uturuki ikiwa  ni  sehemu  ya  uchunguzi  kuhusiana na  madai  ya  ujasusi  na udukuzi  dhidi  ya  Waziri  Mkuu Tayyip Erdogan   na  watu  wake  wa  karibu  katika serikali.

Kufuatia uchunguzi huo, kiasi  cha  maafisa  polisi  20  wamekamatwa katika  majimbo  13  nchini  humo.

Katika  mwezi  uliopita , maafisa wengine wapatao 50  walikamatwa  kwa madai ya  kuunda  ushirika  wa  kihalifu  na udukuzi  wa  simu, ikiwa  ni  sehemu  ya  kile  Waziri  Mkuu Erdogan  alichosema  kuwa  ni  taifa  sambamba  ambalo linapanga  njama  dhidi  yake.

Hatua  hiyo  ya  kuwakamata maafisa  wa  polisi  inakuja wakati Erdogan  ameshinda uchaguzi  wa  kwanza  wa rais nchini  humo  ambapo  rais anachaguliwa  moja  kwa  moja  na  wananchi Agosti  10.


No comments:

Post a Comment