CANBERRA
Serikali
ya Australia imesema kuwa baadhi ya
watoto katika vituo vinavyowahifadhi wahamiaji
nchini Australia wataachwa huru.
Kiasi
ya watoto 150 na familia zao ambao
wamewasili nchini humo kabla ya sheria kali
za uhamiaji kuanza kutumika Julai 2013, wataruhusiwa
kuishi katika jamii wakati maombi yao
ya hifadhi yakishughulikiwa.
Hata
hivyo, mamia ya watoto wengine walioko
nchini humo na wengine nje ya nchi hiyo
katika vituo vya kuwahifadhi wataendelea kubaki
katika maeneo hayo.
Waziri
wa uhamiaji wa Australia, Scott Morrison, amesema
sera ngumu za uhamiaji nchini humo ni
muhimu ili kuwazuwia watu kufanya safari
hatari za maboti kwenda nchini humo.
Makundi
ya kutetea haki za binadamu yanakosoa hatua
ya kuwaweka watoto katika vituo hivyo
wakisema inaathiri afya yao kiakili na kimwili.
No comments:
Post a Comment