Wednesday, August 20, 2014

WAPIGANAJI WA TALIBAN WAWASHAMBULIA WANAJESHI WA AFAGHANISTAN



KABUL

Wapiganaji  wa  Taliban  wamewashambulia wajeshi wa jeshi la Afghanistan  na  vituo  vya  upekuzi  barabarani vilivyowekwa  na  polisi  katika  jimbo moja karibu  na  mji mkuu  Kabul, wakati  nchi  hiyo  ikisherehekea siku  ya uhuru.

Mkuu  wa  baraza  la  mji  wa Logar, Abdul Wali, amesema  kuwa  wapiganaji  wapatao 700 wa  Taliban wameshambulia  vituo  vya  upekuzi  barabarani  katika wilaya  ya  Charkh   

Amesema wapiganaji  20  wa  Taliban  na  mwanajeshi  mmoja wameuwawa  katika  mashambulii hayo.

Taliban  pia  wamethibitisha  kutokea  mapigano hayo, hata hivyo bado haijatoa takwimu kwa waliouwawa.

No comments:

Post a Comment