Madaktari bingwa wanne kutoka Misri wamewasili
nchini kwa ajili kubadilishana uzoefu, ujuzi, kupanua wigo na kukuza uhusiano
katika kitengo cha Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) ikiwa ni kampeini ya afya
na upasuaji.
Madaktari hao ni Mohamed Bigirmy, Ezzat Kamel,
Tamer Ahmed na Hussein Mohamed watakaosaidiana na madaktari wa Tanzania katika
kampeini hiyo.
Ujio wa madaktari hao, uliratibiwa na Mashirika
ya Kimataifa ya African Relief Committee of Kuwait na Al-Rahma International
yanayohusika na utoaji wa misaada na huduma kwa jamii, kwa kushirikiana na
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, Mratibu wa kampeni hiyo, Khamis Mkanachi aMEsema madaktari hao kutoka
Misri wameanza kampeni hiyo jana mpaka Agost 18.
Naye, Mkurugenzi wa MOI, Othman Kiloloma ameishukuru
wizara ya afya kwa kuwaleta madaktari hao watakaosaidia kupunguza changamoto ya
upungufu wa madaktari bingwa katika kitengo hicho ambacho hadi sasa wapo watano
tu kwa uwiano wa daktari mmoja wagonjwa wengi.
No comments:
Post a Comment