Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umemtaka
Rais Jakaya Kikwete kusimamisha shughuli za Bunge Maalum la Katiba na
kusikiliza matakwa ya wananchi kwa maslahi ya kupata katiba itakayokuwa na
manufaa ya wananchi wote na taifa kwa ujumla
Hayo
yameelezwa na viongozi wa umoja huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James
Mbatia, wakati wakizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam .
Viongozi
wa umoja huo wamesema kuachwa kuendelea kwa shughuli za bunge hilo kutapelekea
kupotea kwa fedha za wananchi bila kuzingatia ridhaa zao jambo ambalo halitakua
na tija kwa taifa la Tanzania.
Aidha,
wamemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi
maalum kwenye matumizi ya fedha za Bunge hilo ili kudhibiti suala la ufisadi.
Kwa
upande wake Mbatia amesema wajumbe wa bunge hilo hawanabudi kuzingatia matakwa
ya wananchi ili kujipatia katiba itakayokuwa na manufaa kwa watanzania wote
No comments:
Post a Comment